February 6, 2017


Cameroon imeonyesha inaweza baada ya kuishinda Misri kwa mabao 2-1 katika mechi ya fainali na kubeba ubingwa wa Afcon.

Leo ndiyo mwisho wa michuano ya Afcon na Cameroon ambayo haikupewa nafasi sana imekwenda nyumbani na kombe hilo.


Misri ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Mohamed Elneny katika dakika ya 22, bao hilo likadumu hadi mapumziko.

Cameroon walisawazisha bao lao katika dakika ya 59 mfungaji akiwa Nicholas Nkoulou kwa kichwa na Vicent Aboubakar akafunga bao safi katika dakika ya 88 na kukamilisha ndoto ya Cameroon kubeba ubingwa huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV