February 6, 2017


Mohammed Matumla amepigwa na kuumizwa vibaya hali iliyosababishwa akimbizwe hospitali ya Temeke kwa kutumia gari dogo la mizigo au pick up.


Matumla ambaye ni mtoto wa bondia nyota wa zamani, Rashid Matumla amepigwa katika raundi ya saba na bondia Mfaume Mfaume.

Pambano lao lilikuwa la utangulizi lililokuwa likisubiriwa kwa hamu zaidi leo.


Matumla alianza kupoteza mwelekeo katika raundi ya tano lakini akajitutumua hadi raundi ya saba ambayo aliambulia kipigo kikali kutoka kwa Mfaume.


Baada ya kusukumiwa ngumi mfululizo, alianguka lakini akaonekana ni kama mtu aliyechanganyikiwa, akitaka kukimbia. wakamuhi na kumzuia na baadaye kumlaza chini.


Daktari aliyekuwa mtazamaji, ndiye alilazimika kumtibu kwa ajili ya huduma ya kwanza kwa kuwa hakukuwa na huduma ya kwanza wala gari la wagonjwa ukumbini hapo.Wakati anaondolewa ukumbini hapo, hali yake haikuwa nzuri na alikimbizwa katika hospitali ya Temeke.

2 COMMENTS:

  1. Huo mchezo bongo sio kizazi hiki, maana hata vitu muhimu endapo mtu akizidiwa hakuna. Ukicheza huo mchezo sawa tu unajaribu bahati ya nasfi yako vitani

    ReplyDelete
  2. Huo mchezo bongo sio kizazi hiki, maana hata vitu muhimu endapo mtu akizidiwa hakuna. Ukicheza huo mchezo sawa tu unajaribu bahati ya nasfi yako vitani

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV