February 5, 2017Mashabiki Simba wamemshauri kocha wao, Joseph Marion Omog kuendelea kumtumia zaidi na zaidi mshambuliaji Laudit Mavugo.

Mashabiki hao wanaamini kama Omog ataendelea kumtumia Mavugo, maana yake atajenga  hali ya kujiamini na kuendelea kufunga.

Mavugo alifunga bao la tatu wakati Simba ikiinywa Majimaji kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea, jana.

Wengi wa mashabiki waliotuma maoni yao kupitia salehkubwa@gmail.com walisisitiza Omog kutobadili uamuzi wake kwa Mavugo.

“Mavugo anatakiwa aendelee kucheza, mwambieni Omog tunamuunga mkono lakini asikate tamaa na Mavugo,” alisema Mohammed Saidi wa Masasi.

“Shida ya Omog hamuamini Mavugo, abadilike,” alisema Joseph Mkandile aliyeandika kutoka Mbeya.

Said Mkamba wa Singida, alisema: “Mavugo hajazoea ligi ya Bongo. Kocha ampe nafasi tena na tena naamini atabadilika na kufunga mfululizo. Angalia Yanga, Chirwa anapewa nafasi kila mara, mwisho kazoea.”

Wengi walionekana kuweka maoni yao katika suala la Mrundi huyo kupata nafasi zaidi kwa kuwa anaonekana ana vitu lakini amekuwa hapati muda wa kutosha.


Kati ya watu 72 waliotuma maoni yao, 66, walionekana kutaka Mavugo apewe nafasi zaidi. watatu wakataka Mavugo naye ajitume zaidi. Lakini waliobaki, wao walisisitiza kufurahishwa na Simba kubadilika na kuanza kufunga mabao mengi huku wakishambulia sana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV