February 3, 2017







Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limetangaza Serengeri Boys kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17.

Caf imeitangaza Tanzania kupitia Serengeti Boys na kuing’oa Congo iliyofuzu lakini ikawa na tuhuma ya kumchezesha mchezaji kijeba Langa Bercy ambaye imeelezwa anacheza Ligi Kuu ya Congo.

Ilitakiwa Congo kumpeleka mchezaji huyo kwa ajili ya vipimo vya DNA ili kubaini umri wake kitaalamu.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas Mapunda amethibitisha hilo: "Ni kweli tumepata taarifa hizo za Caf kwamba Congo wametolewa nje. Tanzania sasa imefuzu."


Lakini mwisho ilionekana suala hilo lilishindikana na mwisho usiku huu, Caf imetangaza rasmi kuwa Serengeti Boys au Tanzania ndiyo iliyofuzu michuano hiyo ya vijana Afrika.

Katika mechi ya mwisho, Serengeti Boys ilifungwa bao 1-0 ikiwa ni baada ya kushinda 3-2 nyumbani Dar es Salaam na mfungaji wa bao la Congo nyumbani kwao akiwa ni kijeba huyo aliyekuwa amekomaa sura ile mbaya lakini akachezea timu ya watoto.

3 COMMENTS:

  1. Huo ulikuwa wizi mubashara. Tunaishukuru caf kwa kutenda haki pia TFF kwa kugundua na kufuatilia suala hilo

    ReplyDelete
  2. Ni muda wa kujianda sasa serengeti boys taifa linawategemea

    ReplyDelete
  3. Ni muda wa kujianda sasa serengeti boys taifa linawategemea

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic