February 10, 2017Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja ameibuka na kusema kuwa ili waweze kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu ni lazima wawafunge watani wao, Yanga katika mchezo wao wa Februari 25, 2017.


Amedai kuwa kinyume na hapo itakuwa ni sawa na kuwaachia wapinzani wao hao nafasi ya kuufuata ubingwa.


Yanga na Simba zinatarajia kukutana katika raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara ambapo raundi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.


Mayanja amesema wanahitaji kushinda mechi hiyo ili kujihakikishia nafasi ya kutwaa ubingwa, licha ya kuwa hata michezo mingine nayo ina umuhimu.


“Kwa sasa ligi ilipofikia ni hatua muhimu sana kwani hadi sasa inaonyesha ni timu mbili tu ndizo zinazowania kutwaa ubingwa ambazo ni Simba na Yanga, huku timu zinazotarajia kushuka daraja zikionekana wazi.


“Hivyo, tunahitaji kupigana ili kuweza kushinda mechi zetu zote zilizo mbele yetu, lazima tuifunge Yanga na iwapo tutawaachia wakatufunga na wakaendelea kushinda mechi zao zote itatuwia vigumu kuweza kutwaa ubingwa.


“Lengo letu ni  kuona tunafanikiwa kufanya vizuri katika mechi zetu zote, kwa kukiandaa vizuri kikosi kwani kwa sasa tupo katika ushindani wa hali ya juu kila timu inapigana ili kuweza kushinda, tunahitaji kujipanga vilivyo kuweza kutwaa ubingwa msimu huu,” alisema Mayanja.Aidha, aliongeza kuwa hatua ilipofikia ligi hivi sasa ni ya muhimu na inahitaji upambanaji wa hali ya juu kwa kuwa tayari kasi ya Simba na Yanga ni kubwa kuliko timu nyingine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV