Kocha Mkuu wa timu ya Soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’,
Salum Mayanga amekabidhi programu ya miezi sita kwa Mkurugenzi wa Ufundi wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi akianzia mechi ya
kirafiki za kimataifa kabla ya mechi za ushindani.
Mechi hizo ni kwa za wiki kwa mujibu wa Kalenda ya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na kalenda ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ambako kwa kuanzia tu, ataanza maandalizi ya mechi
za wiki ya FIFA ambazo zitachezwa kati ya Machi 21 na 29, mwaka huu.
TFF bado inaratibu michezo dhidi ya Taifa Stars
inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro kwa maana ya wapinzani wao hapo baadaye.
Mwezi Aprili, kati ya tarehe 20 hadi 22, 2017 kutakuwa na
mechi za kufuzu kwa michuano ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika kwa wachezaji wanaokipiga Ligi ya Ndani (CHAN) ambako Taifa Stars
itacheza na Rwanda katika hatua za awali. Fainali za CHAN zitafanyika Kenya
mwakani.
Kwa mujibu wa ratiba, Juni 6 hadi 13, mwaka huu kutakuwa
na mechi za kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya
Lesotho katika mchezo utakaofanyika hapa Tanzania.
Kwenye AFCON Tanzania iko kundi “L” ambalo wapinzani wake
wako Lesotho watakaoanza kucheza nao hapa nyumbani kabla ya huko mbele kucheza
na Uganda na Carpe Verde. Fainali za AFCON zinatarajiwa kufanyika Cameroon,
mwaka 2019.
0 COMMENTS:
Post a Comment