February 5, 2017
Pamoja na Ruvu Shooting kuendelea kufulia kwenye Ligi Kuu Bara, Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ameendelea kutamba kwamba wataibuka na akisisitiza watafanya yao katika mechi yao dhidi ya Toto Africa, kesho.


Bwire amesema wanakwenda Kirumba jijini Mwanza, kesho kung'oa meno ya mtoto Toto.


"Ndugu yangu, sisi tuko vizuri na soka letu ni safi na la kuvutia. Kinachoendelea ni sehemu ya matokeo ya mchezo.


"Lakini kesho pale Kirumba tutang'oa meno ya mtoto Toto kutoka kinywani mwake," alisema.


Ndani ya mechi tatu, matokeo ya Shooting yamekuwa ya kuyumba huku msemaji huyo akionekana kutokata tamaa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV