February 8, 2017



Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kesho amepanga kwenda kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi cha jijini Dar es Salaam maarufu kama "Sentro" kesho badala ya keshokutwa .

Manji ameyasema hayo hivi punde saa chache tangu Mkuu wa Mkoa wa Polisi wa Dar es Salaam , Paul Makonda kutangaza majina 65 ya wanaitakiwa kufika kwenye kituo cha hicho kikubwa cha Polisi ili kusaidia vita ya kupambana na madawa ya kulevya kama sehemu ya wanaotumihumiwa au la.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Manji alisema kuwa  hawezi kubadili ratiba zake keshokutwa na kwenda kupanga foleni ya watu 65 kwa ajili ya kitu hicho.


Manji alisema, ana kazi nyingi za kufanya hiyo keshokutwa ijumaa, hivyo ataenda kesho asubuhi na mapema sana ili kutekeleza suala hilo aliloitiwa.

Pamoja na kukubali kwenda tena mapema, Manji amesema amepanga kuchukua hatua za kisheria kwa kwenda mahamakani kwa ajili ya kumfungulia mashtaka Makonda.

"Mimi nitaenda kituo cha Polisi kesho asubuhi na mapema na sisubiri hiyo Ijumaa anayotaka yeye Makonda naomba nieleweke.


"Baada ya kutoa huo ushirikiano Polisi, basi nitaenda mahakamani kumfungilia mashtaka Makonda kwa kunidhalilisha kwa kutumia vibaya jina langu, kwani kitendo cha kutumia jina la mtu vibaya ni makosa na katiba ya nchi inaniruhusu kumshtaki Makonda," alisema Manji.

"Kama kweli mtu unamuita kukusaidia kwa ajili ya madawa ya kulevya, vipi unamtangaza mbele ya hadhara. Akishakutajia utaweza vipi kumlinda muda wote, ingekuwa vizuri kumuita kimyakimya, halafu akutajie na wewe ufanyie kazi hasa kama uliona anajua," alisema.

"Kweli nitakwenda Alhamisi, niko tayari kupimwa na kusachiwa. Lakini ningependa na Makonda apimwe pia na kusachiwa.

"Sikatai kuwepo na vita ya madawa, lakini hauwezi ukafanya kila kitu bila ya kujali haki za watu, heshima zao, majina yao. Hii si sawa na siwezi kukubali."



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic