Masau Bwire amesema kikosi cha Ruvu Shooting kimechoshwa na vipigo.
Bwire ambaye ni msemaji wa kikosi hicho amesema wamejipanga kushinda mechi zijazo ili kuepusha kuwaumiza mashabiki wao.
“Hakika tumechoka kuwaumiza mashabiki na sasa tunataka kufanya vema.
“Wengi wameona uwezo wetu ndugu yangu lakini wanashangazwa kabisa na namna tunavyoshindwa kufanya vibaya,” alisema.
“Tumewaahidi sasa tutacheza vizuri na kushinda na si kucheza tu,” alisisitiza Bwire ambaye kikosi chake kimekuwa na mwendo wa kusuasua.
0 COMMENTS:
Post a Comment