February 1, 2017




Baada ya kuachana na SønderjyskE na Denmark, Emmanuel Arnold Okwi amerejea katika klabu yake ya zamani ya SC Villa.

Amejiunga na timu hiyo hadi mwisho wa msimu huu ambayo ni takribani miezi mitatu ijayo huku akisema yuko tayari kuanza kazi.

Okwi amesema atahakikisha anaisaidia Villa iliyomkuza kufanya kweli.

“Niko tayari, nataka kufanya vizuri na kuisaidia Villa,” aliiambia Kawowo ya Uganda.

Kumekuwa na taarifa kwamba Okwi yuko Dar es Salaam akitaka kujiunga na Simba.


Lakini Okwi amekuwa akisisitiza ameelekeza nguvu zake kuifanyia Villa kazi wakati akisubiri kujua kinachofuatia.

1 COMMENTS:

  1. Simba wamrudishe okwi msimu ujao aje awanyooshe hawa hawa vyura wanaojiita wakimataifa ila uwezo mdogo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic