Stand United wamelalama kwamba mwamuzi Alex Mahagi amewadhoofisha katika mechi yao iliyopita kwa kutoa adhabu kwa kocha na kipa wao.
Msemaji wa Stand United, Deokaji Makomba amesema kadi nyekundu aliyelambwa kila wao, pamoja na kocha wao kunawadhoofisha kabla ya kukutana na Yanga keshokutwa.
"Kweli tunaumia sana, si sahihi hata kidogo. Kipa namba moja, kapewa kadi ambayo utaona si sahihi, kocha wetu kaondolewa kwenye benchi wakati wanajua tunakwenda kupambana na Yanga.
"Tunaona ni kama kutudhoofisha. Tumeamua kupeleka malalamiko yetu kwenye bodi ya ligi. Lakini msisitizo tunawaomba wawaruhusu kipa na kocha wetu, wawaondolee hizi adhabu.
"Tunajua mwamuzi Mahagi amekosea, ametunyima haki yetu. Lakini hili la kocha na kipa nalo limevuka kipimo, waliangalie hili," alisisitiza.
0 COMMENTS:
Post a Comment