February 9, 2017
Mmoja wa manahodha wa Yanga, Haruna Niyonzima amelishauri Jeshi la Polisi Dar es Salaam kulishughulikia vizuri na kuangalia ubora wa weledi suala la mwenyekiti wao, Yusuf Manji.


Manji ni kati ya watu waliotajwa kwenye listi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wanaotakiwa kwenda kuhojiwa na Polisi Kesho. Lakini yeye amesema atakwenda kesho kujibu tuhuma hizo za madawa ya kulevya.

Niyonzima raia wa Rwanda amesema ameshangazwa kuona Manji anahusishwa na madawa ya kulevya.

“Yeye ndiye alikuwa anatukataza, sasa leo ukisema ndiye anayefanya ni ajabu sana. Alisema tukae mbali na mambo hayo ili kujiweka vizuri kimaendeleo,” alisema.

“Kama wameona kuna tuhuma, vizuri wakashughulikia kwa kufuata usahihi. Unajua Manji ndiye mtu anaingoza vita ya Yanga, akipata matatizo na hasa vitu ambavyo hafanyi, basi inatuathiri pia hata sisi.

“Tunaamini hili litashughulikiwa na kwenda sahihi badala ya kwenda kwa maoni au muono wa mtu binafsi,” alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV