February 1, 2017Simba imepata pigo baada ya beki wake kisiki, Abdi Banda kutakiwa kukaa nje kwa siku 10 kwa ajili ya kupumzisha mwili sambamba na kuuguza majeraha yake ya misuli aliyoyapata hivi karibuni,.


Kutokana na hali hiyo sasa beki huyo atakosa mchezo ujao wa timu hiyo dhidi ya Majimaji lakini akiaminika kuwa ataweza kucheza mechi dhidi ya Yanga, Februari 25.


Banda amegeuka lulu kwenye safu ya ulinzi ya Simba inayonolewa na Mcameroon, Joseph Omog alipata majeraha hayo ya misuli baada ya kufanya mazoezi magumu kwa kipindi cha miezi miwili ambapo sasa amewekwa nje kwa ajili ya kuifanya misuli hiyo iachie.


Banda amekiri kutokuwa sehemu ya timu hiyo inayojiandaa na mechi ya Majimaji baada ya kupewa siku za kupumzika kutokana na majeraha hayo ya misuli.


“Mimi nipo nyumbani nimepewa siku 10 za kupumzika kwa ajili ya kupoza misuli yangu ambayo ilikaza baada ya kufanya mazoezi magumu kwa miezi miwili mfululizo.“Wakati nikiwa nje ya timu nitakosa mechi hii inayokuja dhidi ya Majimaji na muda wote huo nitakuwa naenda hospitali kwa ajili ya kupatiwa tiba ya tatizo langu,”alisema Banda.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV