February 17, 2017Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetuma salamu za rambirambi kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya kutokana na kifo cha mchezaji wa zamani Tanzania Prisons, Young Africans na timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’.


Taarifa kutoka Mbeya, zilizothibitishwa na uongozi wa Mkoa zinasema kwamba mchezaji huyo alifariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa Februari 17, 2017 kwenye Hospitali ya Wilaya ya Rungwe.


TFF itawakilishwa na Katibu wa Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya, Seleiman Haroub ambaye kwa sasa atashirikiana na familia kufanya taratibu za mazishi ambayo taarifa zaidi zitatangazwa baadaye mara baada ya vikao vya uamuzi.

Katika salamu zake za rambirambi, TFF imewataka ndugu wa marehemu kuwa na uvumilivu kwa kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito kwa Bonny ambaye nyota yake iling’ara zaidi wakati Taifa Stars inafundishwa na Mbrazil Marcio Maximo.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV