February 15, 2017



Simba inataka pointi tatu katika kila mchezo kuhakikisha inatwaa ubingwa.


Lakini Kesho Alhamisi itakuwa ni siku ya kutaka kuua ndege wawili kwa jiwe moja. Lengo ni kuhakikisha inaishinda African Lyon ili kupata pointi tatu lakini kulipa kisasi cha kufungwa.

African Lyon ilikuwa timu ya kwanza kutibua rekodi ya Simba inayonolewa na Kocha Joseph Omog kwa kuichapa bao 1-0. Hii ilikuwa ni mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.

 Lakini mechi ya kesho ni ya Raundi ya Sita ya kuwania Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) yaani Azam Sports Federation Cup.

Mchezo huo awali ulipangwa kufanyika Machi Mosi, 2017 lakini ulirudishwa nyuma kwa sababu za kiufundi kutoka timu zote mbili.

Michuano ya raundi hiyo ya sita, itaendelea tena Februari 24, mwaka huu kwa michezo minne kuchezwa kwa siku hiyo kuanzia saa 10.00 jioni kasoro mchezo mmoja tu utakaochezwa saa 1.00 jioni.

Michezo ya siku hiyo kwa mujibu wa ratiba inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), itakuwa ni kati ya Madini FC ya Arusha na JKT Ruvu ya Pwani watakaocheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Kagera Sugar itacheza Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mechi nyingine itakuwa ni kati ya The Mighty Elephant ya Ruvuma na Ndanda FC ya Mtwara zitakazopambana kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea ilihali Azam na Mtibwa Sugar watacheza Chamanzi –Mbagala – mchezo utakaofanyika saa 1.00 usiku.

Jumapili Februari 26, mwaka huu timu ya Mbao FC itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City zote za Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Machi 7, mwaka huu Young Africans SC itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic