February 4, 2017Siri imefichuka, kumbe Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimpunguzia mshahara aliyekuwa Kocha wa Taifa Stars, Charles Mkwasa, mbaya zaidi hata huo waliokubaliana TFF ilishindwa kumlipa na sasa kocha huyo anataka kwenda Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ili kushinikiza alipwe deni lake.

Mkwasa ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Yanga, alipewa jukumu la kuinoa Taifa Stars baada ya kutimuliwa kwa Mart Nooij raia wa Uholanzi ambaye alikuwa akilipwa Sh milioni 28 kwa mwezi.


Mkwasa alisema wakati akiinoa Taifa Stars alikubaliana na TFF kupunguza mshahara wake lakini hata baada ya kufanya hivyo, shirikisho hilo lilishindwa kumlipa na kujikuta likiweka deni la Sh milioni 80 hadi sasa.

“Hadi sasa sijalipwa fedha yoyote na TFF katika kile kiasi ninachodai, kwanza nilipunguza mshahara kwa makubaliano nao lakini hata huo tuliopunguza hawakunilipa na kuweka deni hilo.


“Kama hali ikiendelea kuwa hivi, nitapeleka malalamiko yangu Fifa ili nilipwe haki zangu kwa maana naona hakuna dalili za kulipwa licha ya kuweka mikakati kadhaa ya kunilipa ikiwemo kulipwa nusu kwanza.


 “Kwa sasa naendelea kuwasikilizia nione lini watanilipa, kama wakiendelea kukaa kimya basi nitaenda kuwashtaki Fifa ili haki yangu niipate haraka,” alisema Mkwasa.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV