February 9, 2017Bado viongozi wa Yanga wamepigwa na butwaa na hawajui Mwenyekiti wao Yanga, Yusuf Manji yu wapi.

Hadi saa tatu na nusu usiku, baadhi ya maofisa wa Yanga walikuwa katika Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam, wakihoji alipo Manji.

Manji pamoja an na Mchungaji Josephat Gwajima walipakiwa kwenye gari la Polisi aina ya Toyota Landcruiser lenye rangi nyeupe, ilikuwa kama saa 10 na nusu jioni.

Gari hilo lenya usajili namba T 213 ARS liliondoka kituoni hapo kuelekea Posta ya zamani na haijajulikana hadi sasa walipelekwa wapi na hawakuwa wamrejeshwa kituoni hapo.

Baadhi ya maofisa wa Yanga, wamezungumza na SALEHJEMBE na kusema hawajui alipo mwenyekiti wao na wengine wakiamini alipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na wengine wakidai huenda yuko nyumbani kapumzika.

“Ukweli alipo hakuna anayejua. Hakuna uhakika na kila mmoja anasema lake,” alisema mmoja wa maofisa wa Yanga.

Mwingine ambaye ni msaidizi wa Manji alisema: “Si unaona hadi sasa tupo hapa (kituoni), hatujui bosi wetu alipo. Maana tokeo ameondoka hiyo jioni hatujamuona na hajarudi.”

Manji na Gwajima, wote wako kwenye listi ya watu 65 iliyotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwa wanashukukiwa kutumia au kusambaza madawa ya kulevya.

Hivyo kutakiwa wafike kituoni hapo kesho lakini wao wawili waliamua kufika leo.

Leo mchana, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Simon Siro alisema hawezi kulizungumzia suala hilo hadi kesho mchana, angalau kuanzia saa sita mchana.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV