February 11, 2017


Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amefungua mdomo wake na kusema umefikia wakati watu wakapunguza tabia ya kulalama kupindukia.

Wenger amesema wengi wamekuwa wakimlaumu kiungo Mesut Ozil kuwa hana msaada lakini hawana sababu za msingi kwa kuwa wanabagua.

“Timu ikishinda ni furaha ya wote, ikifungwa watu wanaanza kubagua wachezaji na kuwalaumu baadhi, mfano Ozil. Si sahihi, vizuri watu wakawa waungwana na kuangalia hali halisi ilivyo,” alisema.


Mashabiki wa Arsenal wakiwemo wa Tanzania wamekuwa wakilalama kuhusiana na timu yao kutofanya vema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV