Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amekimbizwa hospitali baada ya kuugua akiwa mahabusu.
Taarifa zinaeleza, Manji ambaye alikuwa mahabusu katika kituo Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam, alianza kuumwa tokea jana.
“Kweli amekimbizwa hospitali na sasa anapatiwa matibabu,” alisema mmoja wa watu wake wa karibu.
Manji alikuwa mahabusu ambako amewekwa tokea Alhamisi iliyopita baada ya kuitwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akitajwa katika listi ya watu 65 wanaotuhumiwa katika suala la madawa ya kulevya.
Kumekuwa na taarifa huenda kesho akafikishwa mahakamani, lakini bado maofisa wa Jeshi la Polisi wamekuwa hawataki kulizungumzia suala hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment