February 12, 2017


MPIRA UMEKISHAAAA
Dk 89, Yanga wanaendelea kushambulia kwa kasi, Chirwa anaingia lakini Mohamed Zahir anamzuia hapa
Dk 88, Makapu anafanya kazi ya ziada kuukoa mpira kutoka kwa Said aliyekuwa ameingia vizuri
Dk 87, Zulu tena, anajaribu shuti la mbali na mpira unaokolewa na mabeki wa Ngaya


Dk 84 Yanga wanaingia vizuri, pasi ya Kamusoko, Chirwa anajaribu inawababatiza mabeki wanaokoa
Dk 80, Ngaya wanaingia tena kwenye lango la Yanga lakini Dida anadaka na mwamuzi anasema ni faulo. Juma Abdul anaonekana kuumizwa, anatibiwa hapa
SUB Dk 78 anaingia Said Juma Makapu kuchukua nafasi ya Simon MSuva. Hii inaonekana Lwandamina ameamua kuimarisha kiungo zaidi baada ya kuona Ngaya wanacheza katikati
Chirwa anaingia vizuri tena
Dk 76, Ngaya wanaonekana kuamka na kucheza vizuri katikati lakini bado mashambulizi yao si makali


GOOOOOOOO Dk 73, Kakumusoko anaachia mkwaju mkali kwelikweli unajaa wavuni ilikuwa ni baada ya kupokea pasi ya Niyonzima
Dk 70, Yanga wanaendelea kushambulia kwa kasi na Ngaya wanalazimika kuwa makini lasivyo watakutana na mvua ya mabao
GOOOOOOO Dk 66 Said Khalfan anaachia Mkwaju mkali na kuandika bao kwa Ngaya
GOOOOOOO Dk 65, Tambwe anaunganisha krosi safi ya Juma Abdul na kuandika bao la nne (Mashabiki wa Ngaya wanaanza kuondoka uwanjani)


GOOOOOOOOO Dk 59, Kamusoko anamchambua kipa na kutoa pasi safi kwa Chirwa ambaye anaandika bao saaafi kabisa
Dk 57 kona safi ya Said, mpira unamkuta Juma Abdul, inakuwa kona tena, inachongwa mara ya tatu Cannavaro anaondosha hapa
Dk 56, Alfa anaingia na kupiga mpira krosi hapa lakini Dida anapangua na kuwa kona, inachongwa tena na kuwa kona tena
SUB Dk 56 Nyanga wafanya mabadiliko tena, Ali anatoka na nafasi yake inachukuliwa Derita Alfa

Dk 55, kuna wachezaji wanaingia kumbeba mchezaji aliyeumia wa Ngaya. 
KADI Dk 50, Saidi wa Ngaya analambwa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Kamusoko aliyekuwa ameishamtoka
SUB Dk 48 Ngaya wanafanya mabadiliko Said Haligan anaingia kuchukua nafasi ya Azeraden
Dk 47, Msuva anaingia vizuri tena hapa, anaachia mkwaju mkali hapa lakini Ngaya wako makini
Dk 45 Mpira umeanza, Yanga wanaanza kwa kasi na Msuva anaingia na kuachia mkwaju lakini Goal kick


MAPUMZIKO
Dk 45+2 nafasi nyingine kwa Yanga, kipa akiwa nje ya lango lakini Tambwe anashindwa kulenga na kuwa goal kick
GOOOOOOOOO Dk 45+1, Msuva anaachia mkwaju mkali kutoka pembeni na kuandika bao la pili kwa Yanga
Dk 45, Msuva anaingia vizuri anagongeana na Niyonzima anaachia mkwaju mkali lakini kipa Said Komandoo anaruka na kudaka kama nyani hapa

Dk 44, Tambwe anakwenda vizuri hapa anawekawa chini hapa. Faulo inachongwa na Chirwa lakini Said Komandoo anaudaka kwa mbwembwe hapa
GOOOOOOOOOOOOOO Dk 43, Haji Mwinyi anapiga mpira wa mrefu, Chirwa anauwahi na kupiga pasi safi kwa Zulu ambaye anaachia mkwaju saafi na kuandika bao moja kwa Yanga

Dk 42, hatari kabisa katika lango la Yanga, Dida anaruka kuupiga ngumi mpira, lakini hakuupiga kwa nguvu, ukatua kwa Al Manana, naye akaachia shuti ambalo licha ya kutokuwepo kwa kipa lakini hakulenga lango
Dk 40, krosi nyingine nzuri ya Mwingi, Tambwe anaruka hapa lakini kila Said Komando anaruka na kuudaka vizuri kabisa

Dk 36, Yanga wanaonekana kuwa wepesi na wanapeleka krosi nyingi zaidi lakini mara nyingi kunakuwa hakuna watu wa kuzitumia. Lakini inaonekana hata mabeki wa pembeni wakati wanataka kufunga wao, jambo ambalo linawakosesha nafasi za kufungaDK 35, Yanga wanapata kona nyingine, inachongwa na Niyonzima lakini wanaokoa Ngaya na kuwa wa kurushwa


Dk 31, Tambwe katika nafasi nzuri baada ya kupokea pasi nzuri ya Chirwa, yeye na kipa wa Ngaya aitwaye Komando. Lakini Tambwe anapaishaa juuuu
Dk 30 hatari kwenye lango la Yanga, Fadhul wa Ngaya anaingia vizuri na kuachia mkwaju mkali lakini Dida yuko imara
Dk 29, Niyonzima anachonga kona safi, inaondoshwa. Mpira unamkuta Juma Abdul na kuurudisha kwa Niyonzima na anaachia shuti kali lakini hakulenga
Dk 28, Yanga wanapata kona ya kwanza baada ya krosi safi ya Zulu kuokolewa

Dk 24, Dida anaonyesha umahiri kwa kuuwahi mpira baada ya Cannavaro kuteleza na kuanguka
Dk 18, mpira wa Haji Mwinyi unakwenda juujuu na kugonga mwamba na kutoka nje. Goal kick
Dk 16, krosi nzuri ya Juma Abdul ilitua langoni mwa Yanga lakini mwamuzi amesema ni madhambi
Hata hivyo, Yanga wamekuwa wakijibu mashambulizi hayo kwa mipira ya krosi

Mechi imeanza kwa kasi na Ngaya wamekuwa wakishambulia sana



KIKOSI CHA YANGA
1. Deogratius Munishi 
2. Juma Abdul
3. Mwinyi Haji
4. Nadir Haroub
5. Kelvin Yondani 
6. Justin Zullu 
7. Saimoni Msuva
8. Thabani Kamusoko 
9. Amisi Tambwe
10. Obrey Chirwa
11. Haruna Niyonzima 

Akiba
- Ali Mustafa
- Hassani Kessy
- Oscar Joshua
- Emanuel Martin
- Juma Mahadhi 
- Juma Saidi

- Deusi Kaseke

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic