March 10, 2017



Uongozi wa Azam FC umewaambia wapenzi na mashabiki wa Simba na timu nyingine, waungane kwa pamoja kuishabikia Yanga, kesho Jumamosi itakapocheza dhidi ya Zanaco ya Zambia.

Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd huku akisisitiza kwamba kufanya hivyo ni uzalendo ambao unatakiwa kuanzia sasa na kuendelea.

Yanga itacheza dhidi ya Zanaco katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo mshindi atacheza hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Upande mwingine, Azam FC yenyewe itacheza dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar, ukiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, keshokutwa Jumapili.

“Kwa sasa lazima tukubali tu kwamba Yanga na Azam ndiyo wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, hivyo litakuwa jambo la busara kwa mashabiki wote kuweka itikadi zetu pembeni na kuuungana pamoja kuhakikisha timu hizi zinafika mbali.

“Nawaomba tu mashabiki wote, wa Azam, Simba na timu nyingine Jumamosi tukaishangilie Yanga pale Taifa, kisha Jumapili, tuungane tena kwenda Azam Complex kuishangilia Azam,” alisema Idd.


1 COMMENTS:

  1. Ni rahisI chama tawala Africa kukubali kimeshindwa uchaguzi...walikataa vs mazembe ambapo ilikuwa bure ikawe hii????

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic