March 10, 2017



Kiungo mwenye kasi wa Mbeya City, Mrisho Ngassa, amefunguka kuwa yupo mbioni kuachana na klabu yake ya sasa ya Mbeya City mara baada ya kumalizika mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.

Ngassa alijiunga na Mbeya City katika usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea Fanja FC ya Oman, amesema mkataba ukiisha amepanga kuondoka kwenda Oman.

“Mkataba niliosaini hapa (Mbeya City) ni wa muda mfupi, hivyo sitarajii kuongeza mwingine. Niliondoka Fanja kwa sababu kibali changu kilikuwa na matatizo na ndiyo maana nilirudi hapa Bongo, lakini mipango yangu ikikaa sawa nitarejea kule,” alisema Ngassa.


Ngassa alijiunga na Fanja akitokea Free State Star ya Afrika Kusini ambayo alivunja nayo mkataba na kwenda Oman.

Lakini kabla, akiwa hapa nchini Ngassa alianza kuonyesha cheche akiwa na Toto Africans ya kwao Mwanza kabla ya kujiunga na Kagera Sugar na kuonyesha uwezo mkubwa na kuivutia Yanga.

Timu nyingine kubwa alizozichea baada ya Yanga ni Simba ambayo alijiunga nayo akitokea Azam FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic