March 27, 2017



Baada ya  tetesi zilizojitokeza hivi karibuni kuwa uongozi wa Yanga upo katika mipango ya kuwachukua wachezaji wa Simba, kiungo Jonas Mkude na mshambuliaji Ibrahimu Ajibu,  mabosi wa wachezaji hao wameibuka na kusema kuwa ni ruksa kwa kuwa wachezaji hao wapo huru kufanya chochote kutokana na mikataba yao kukaribia kufikia tamati.

Kuna taarifa kuwa tayari kuna mipango imeanza kufanywa ndani ya Yanga kuhakikisha wanawapata wachezaji hao kutokana na majina yao kutajwa kuwepo katika mchakato wa kusajiliwa msimu ujao wa ligi kuu kufuatia mikataba yao kumalizika  huku Ajibu akitajwa kuwa katika rada zao kwa  muda mrefu.

Aidha, Mkude na Ajibu ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajia kumaliza mikataba ndani ya Simba mwezi wa sita mara baada ya ligi kufikia tamati ambapo hadi sasa wamegoma kufanya mazungumzo ya kuongeza mkataba mwingine wa kuitumikia timu hiyo kwa madai kuwa wanasubiria hadi watakapomaliza rasmi mikataba yao mwishoni mwa ligi ndipo wafanye maamuzi.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alisema kuwa, iwapo kuna watu wanafanya mazungumzo na wachezaji wao hao waendelee kwa kuwa hawawezi kuwazuia kwa kuwa ni wachezaji huru ambao mikataba yao inakaribia kumalizika.

“Kama kuna watu wanafanya nao mazungumzo waache tu waendelee kuzungumza nao, mimi sijui chochote, watu wamekuwa wakiniuliza sana kuhusiana na jambo hilo, kwa upande wetu muda bado wa kuweza kuzungumzia suala hilo, ila tunachojua bado ni wachezaji wetu na hawajamaliza mikataba yao hadi mwisho wa ligi.

“Kwa sasa Ajibu na Mkude ni wachezaji huru popote wanaweza kwenda kama Yanga wamefanya nao mazungumzo ni sawa, kwani mchezaji akiwa anakaribia kumaliza mkataba anakuwa huru hivyo ni ruksa kuzungumza na timu nyingine, kusema watu wa Yanga wanawahitaji mimi hainihusu na wala siwezi kuwazuia, ni ruksa kwenda kokote.


“Kwa sasa mtazamo wetu wote ni kwenye ligi na tutakapofikia huko tutasema kinachoendelea, wakati wa usajili bado,” alisema Hanspope.

3 COMMENTS:

  1. Hanspoppe leo unaongea hivyo lakini wakijiunga na yanga unaanza kulalamika mara ooh wale ni bado wanamikataba na simba. Hatutaki maneno yako hayo.

    ReplyDelete
  2. Hanspoppe leo unaongea hivyo lakini wakijiunga na yanga unaanza kulalamika mara ooh wale ni bado wanamikataba na simba. Hatutaki maneno yako hayo.

    ReplyDelete
  3. Sasa Juma Masudi ulitaka ajibu vp wakati ukweli ndio huo..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic