BEKI wa pembeni wa Yanga, Juma Abdul amesema hataki kubishana na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliani wa Simba, Haji Manara na badala yake yeye atamuonyeshea kwa vitendo ndani ya uwanja.
Kessy aliitoa kauli hiyo mara baada ya mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa juzi Jumatano na Yanga kufanikiwa kuibuka kwa ushindi wa mabao 2-0 huku beki huyo akianza kwenye kikosi cha kwanza cha Mzambia, George Lwandamina.
Beki huyo, tangu atue kuichezea Yanga hakuwa na nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo na mara kadhaa amekuwa akitokea benchi katika timu hiyo.
Kessy amesema aliiona na kuisoma ‘post’ ya Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram ambayo ilikuwa ikimdhihaki kutokana na kukaa benchi.
Kessy alisema baada ya kuisoma hakutaka kumjibu na badala yake alikaa kimya kuhofia majibizano yasiyokuwa na maana na badala yake akili zake alizielekeza kwenye kucheza soka pekee.
“Hivi vitu vinavyotokea hivi sasa kutoka kwa viongozi wa Simba akiwemo huyo Manara nilivitarajia tangu natoka Simba ninakuja kuichezea Yanga.
“Nakumbuka mwanzoni wakati nasaini kuichezea Yanga nilikuwa najibizana nao kwenye vyombo vya habari, lakini baada ya kugundua kuwa ninatoka mchezoni ninapojibizana nao, nikaamua kukaa kimya.
“Hivyo, sitaki kumkaribisha ibilisi hivi sasa na badala yake nitakaa kimya nikifanya kazi yangu ndani ya uwanja kwa kuwajibu kuonyesha kiwango kikubwa kwa lengo la kuipa ubingwa timu yangu ya Yanga,” alisema Kessy.
0 COMMENTS:
Post a Comment