March 3, 2017Mechi wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga uliochezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ulikusanya kiasi cha fedha cha shilingi milioni 324.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, amesema mapato hayo yamepatikana baada ya kupiga hesabu za mashabiki waliojitokeza kutazama pambano hilo.


“Mechi ya Simba na Yanga imeingiza kiasi cha shilingi milioni mia tatu ishirini na nne laki moja na themanini, hiyo ni baada ya mashabiki wa pande zote kujitokeza kuliangalia pambano hilo ambalo lilikuwa na ushindani wa aina yake.


“Kwenye fedha hizo, Simba watapata asilimia 40 (Sh milioni 129.6) ya fedha zote kwa sababu ya uenyeji wao, Yanga wakichukua asilimia 20 (Sh milioni 64.8) ya mapato yote kwa sababu wao walikuwa wageni wa pambano hilo.


“Lakini pia kuna taasisi ambazo zitachukua sehemu ya mapato hayo ambayo ni TFF asilimia 5, VAT asilimia 18, Selcom wao asilimia 5, Baraza la Michezo Taifa (BMT) asilimia 1 na Chama Cha Soka Dar es Salaam (DRFA) asilimia 3.


“Nyingine ni gharama ya uwanja asilimia 15, Bodi ya Ligi (TPLB) wao asilimia 9, gharama ya mchezo mzima ulivyokuwa ikihusisha maandalizi asilimia 7,” alisema Lucas.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV