March 4, 2017MPIRA UMEKWISHAA
-Agyei anaokoa vizuri mpira wa kona na kuwa kona tena.Ungeweza kujaa moja kwa moja, inachongwa tena, anaokoa tena Agyei
-Anaingia Semtawa lakini Simba wanaokoa inakuwa konaaa
-Nchimbi anapiga kichwa safi kabisa lakini Agyei 
-Zahir yuko chini na City wanaonekana kufurahia sare
-City wanaonekana hawajakata tamaa, Simba halikadhalika lakini umiliki, City wanaonekana kuwa na kasi zaidi
- SUB Raphael Bryson anaenda benchi upande wa City, anaingia Zahoro Pazi


DAKIKA 5 ZA NYONGEZA 
Dk 89, Mavugo anapoteza nafasi nyingine nzuri baada ya pasi safi ya Mo Ibra
Dk 87, Mavugo anaingia, vizuri, mpira unaokolewa na kipa na kona lakini haina madhara kwa City
GOOOOOOO Dk 86 Kichuya anapachika bao la pili kwa pelnaltiii
SUB Dk 85 Kabanda analambwa kadi ya njano kwa kumuagusha Zimbwe
Dk 84 Simba wanapata penaaat baada ya ZImbwe kuagushwa na Kabanda
Dk 82 Agyei anafanya ya ziada kuokoa Simba akiwa amebaki yeye na Nchimbi
SUB Dk 80, Simba wanamtoa Ajibu na nafasi yake inachukuliwa na Mwinyi Kazimoto

GOOOOOOOO Dk 79, Kenny Ally anaiandikia Mbeya City bao tena, ni baada ya Simba kuonekana kama wameridhika na sare na wakicheza kwa kujiamini lakini kwenye ukabaji wakiwpuuzia
Dk 76 Simba wanaonekana ni kama waliochoka, upande wa kushoto, Ajibu hakabi wala kuingia ndani ni kama aliyechoka sana. Lakini Semtawa anacheza anavyotaka akiwa anafanya anavyota
Dk 75, Simba wanapata kona baada ya mpira wa Hamadi Juma kuokolewa
Dk 74, Nchimbi anaingia kwa kasi na kuachia mkwaju mkali kabisa, lakini mpira unatoka sentimeta chache pembeni. Ilikuwa hatari 
Dk 71, Simba nao wanapoteza nafasi baada ya Mo Ibra kupiga krosi ambayo inamzidi kasi MavugoDk 70 Raphael anapoteza nafasi nzuri, mpira wake wa kichwa unatoka juu kidogo mwa lango la Simba
Dk 68 sasa, Simba wanaendelea kulishambulia lango la City kama nyuki. Lakini City wanaonekana sasa kuanza kupoteaza muda
DK 65 GOOOOOOO mpira wa adhabu, Ajibu anauchonga kiufundi kabisa na kuandika bao zuri kwa Simba
DK 63 Krosi nzuri ya Kichuya, Mo Ibra na Mkude wanagongana wenyewe
SUB Dk 69, anatoka Ngassa kwa upande wa Mbeya City anaingia Ayoub Semtawa, huyu ni daktari kitaaluma na kati ya wachezaji hatari
Dk 59, Mavugo yeye na lango, baada ya shuti la Mo Ibra kuokolewa, unamkuta Mavugo yeye na lango, anapaishaa buuuuu
Dk 55, krosi maridadi ya Ajibu, inatua kichwani mwa Mavugo lakini anashindwa kulenga lango
SUB Dk 54, Muzamiru anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Mohamed Ibrahim maarufu kama MoDk 52 Kenny Ally naye yuko chini lakini inaonekana kama City wanataka kupunguza makali ya Simba wanaoshambulia mfululizo
Dk 51, nafasi nyingine nzyuri kwa Simba, Ndemla anaachia mkwaju, unaokolewa na kuwa kona, inachongwa, inaokolewa tena kona
Dk 49 Mavugo anabaki yeye na kipa, lakini anashindwa kufunga na mwamuzi anasema tayari aliotea
Dk 48, Simba wanapata kona nyingine, inachongwa na kuokolewa
Dk 47, Simba wanafanya shambulizi kali hapa, Ajibu na Mavugo wanagongeana. Kichuya anaachia shuti kali inaokolewa na kwua kona
Dk 45 Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi, Mbeya City wanataka kuongeza bao la pili na kumaliza mchezo, Simba wanataka kusawazisha MAPUMZIKO
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44 sasa, mpira bado unachezwa katikati zaidi, City wakionekana kutaka kuupoza zaidi na Simba wanataka kufunga
Dk 41, Mbeya City wanapata kona na wanaonekana hawana haraka wakitaka kupoteza muda na ikiwezekana kwenda mapumziko na bao moja
Dk 40, Ajibu anamchambua beki mmoja na Mavugo akiwa katika nafasi nzuri, lakini Ajibu anataka kufunga mwenyewe, kipa Owen anaokoa
Dk 40 Ngassa anawachambua vizuri walinzi wa Simba na kumpa Nchimbi, Agyei anaokpa


GOOOOOOO Dk 37, Nchimbi anaukwamisha mpira wavuni kwa mkwaju mkali kabisa baada ya Raphael Alpha kuuacha mpira nyuma na yeye kuuwahiDk 36, Simba kama wanapoteana hasa katika safu ya ulinzi na wanapaswa kuwa makini
Dk 34, Simba wanaichezea nafasi nyingine ya wazi, Hamadi Juma anapunguza na kupiga krosi safi lakini Muzamiru anabutua tuuuuu
Dk 32, Mavugo anaingia vizuri mbele ya Rajab Zahir lakini unaokolewa na kuwa kona. Inachongwa haina madhara kwa City
KADI Dk 29, Kenny Ally analambwa kadi ya njano kwa kushika mpira lakini akaendelea kulalamika
Dk 25, nafasi nzuri kabisa kwa Mbeya City, Nchimbi kashindwa kutulia na kutoa mpira huo


Dk 23, Simba wanapata kona ya pili baada ya mpira aliokuwa nao kichuya kuokolewa. Inachongwa vizuri na kipa Owen Chaimaa anadaka vizuri kabisa
Dk 21, Simba wanapata mpira wa adhabu nje kidogo nje ya lango la Mbeya City lakini pigo la Ndemla halikuwa na jipya
Dk 17, krosi safi ya Shamte na Kenny Ally anaunganisha kichwa safi, unatoka nje kidogo ya lango la Simba. Lilikuwa shambulizi zuri kwa City
Dk 15, krosi safi hapa ya Hamadi, kipa Owen anafanya kazi nyingine nzuri na kuokoa
SUB Dk 13, Mbeya City wanamtoa Sankan Mkandawile aliyeumia na nafasi yake inachukuliwa na John Kabanda
Dk 12, krosi safi ya Mavugo, Kichuya anapiga kichwa lakini kinakuwa laini na kudakwa na Owen


Dk 10, Simba wanaonekana kuendelea kugongena vizuri na kuutawala mchezo, Mbeya City kama wamesinzia hivi
Dk 7, Kotei anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira mguuni mwa Ditram Nchimbi
Dk 5 pasi nzuri ya Ndemla inatua kwa Mavugo lakini ni offside
Dk 4, Zimbwe alikua anaingia vizuri lakini Shamte anatoa na kuwa kona
Dk 3, Simba wanaonekana kuanza kutulia na kuonana kwa pasi za harakaharaka
Dk 1, mechi imeanza taratibu huku kila upande ukionyesha umepania kufanya vizuri

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV