March 12, 2017


Hofu ya Wanasimba wengi ni mechi tatu za Kanda ya Ziwa ambapo kikosi chao kitacheza katika mikoa ya Mwanza na Kagera.

Tayari kocha Joseph Omog ameonyesha ana matumaini ya kufanya vizuri lakini anaamini wachezaji kadhaa majeruhi watakuwa wamerejea.

Matumaini ya kuwa wamemrejesha Method Mwanjale lakini uhakika wa Juuko Murshid kurejea Ligi Kuu Bara kwa uhakika, tayari upo.

Jamal Simba Mnyate ni kati ya wanaosumbuka na majeraha lakini wakati umesogea na anaweza kuwa fiti kabisa kabla Simba haijamaliza mechi za kanda ya Ziwa.


Simba ndiyo wanaoongoza ligi na wanachotakiwa ni kushinda mechi zake zote zilizobaki ili kutwaa ubingwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV