March 22, 2017Mshambuliaji wa KRG Genk, Mbwana Samatta, rasmi ameanza mazoezi na kikosi cha Taifa Stars.

Samatta amejiunga na Stars usiku wa kuamkia leo baada ya kutua akitokea nchini Ubelgiji.

Chini ya Kocha Salum Mayanga, Taifa Stars imefanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Stars inajiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Botswana Jumamosi na Jumanne ijayo itakuwa ni zamu Burundi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV