March 18, 2017Ili kuhakikisha wachezaji wao wanapona kwa haraka na kurejea uwanjani kuisaidia timu yao, viongozi na mashabiki wa Yanga wameanza mchakato wa matibabu kwa wachezaji Mzimbabwe, Donald Ngoma na Amissi Tambwe raia wa Burundi.


Wachezaji hao, juzi Alhamisi waliondolewa kwenye msafara wa timu hiyo uliokwenda Lusaka, Zambia kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Zanaco.


Ngoma yupo nje kutokana na maumivu ya nyama za paja aliyoyapata kwenye mechi dhidi ya Zanaco wakati awali alikuwa na majeraha ya goti yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu pamoja Tambwe ambaye inadaiwa goti lake limejaa maji.


Taarifa za ndani za Yanga zinaeleza, viongozi na mashabiki wa timu hiyo wamepanga kuwapeleka wachezaji hao nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ya haraka.

Mtoa taarifa huyo alisema, moja ya nchi zilizopendekezwa ni Afrika Kusini na tayari viongozi hao wameanza kuchangishana fedha kwa ajili ya kufanikisha matibabu ya washambuliaji hao tegemeo.


"Tunafahamu kabisa kuwa Ngoma na Tambwe mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu wa ligi kuu, lakini hiyo siyo sababu kwetu sisi tushindwe kuwatibia.


“Kwa sababu wachezaji hao walipata majeraha hayo wakiwa wanaichezea Yanga, hivyo hatuoni sababu ya kuwatibia na kingine tunaamini ni kama fundisho kwa wachezaji wengine wenye mikataba ya kuendelea kuichezea Yanga kama ilivyo kwa akina Ngoma na Tambwe, kikubwa tunataka kujenga uaminifu na moyo wa kuipambania timu yao.

"Hivyo, tumepanga kuwapeleka kuwatibia Sauzi kwani ndiyo nchi ya kwanza tuliyoipendekeza hadi hivi sasa na kikubwa tunataka kuona wachezaji hao wanapatiwa matibabu ya haraka na wanarejea uwanjani wakiwa na nguvu tele," alisema mtoa taarifa huyo.


Daktari Mkuu wa Yanga, Edward Bavu hivi karibuni alisema wachezaji bado afya siyo nzuri na wanaendelea na matibabu huku wakiwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa muda wa wiki moja ili kuhakikisha wanapona kwa haraka.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV