March 3, 2017Taarifa za ndani kutoka Klabu ya Yanga inaelezwa kuwa klabu hiyo imemtimua kazi mkurugenzi wake wa ufundi, Hans van Der Pluijm kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mkakati wa kupunguza matumizi baada ya uchumi wa klabu hiyo kutokuwa katika hali nzuri.

Pluijm, kocha wa zamani wa Yanga alibadilishiwa majukumu ya ukocha na kuwa mkurugenzi wa ufundi, mwaka jana, ameifundisha Yanga katika vipindi viwili kabla ya kubadilishiwa majukumu hayo.Mtu wa uhakika kutoka ndani ya Yanga ameiambia SALEHJEMBE kuwa: “Ni kweli tumeamua kuachana na Pluijm kwa mambo mawili, kwanza hali ya kiuchumi, pili ni kuweka amani ndani ya timu maana mambo yalikuwa mengi, hivyo tumeona bora tuachane naye na katibu mkuu (Charles Mkwasa) ndiye tuliyempa jukumu la kumtaarifu Pluijm kuhusu hali hii.”


“Kubaki na Pluijm ni gharama kubwa na kama unavyoona hali ya uchumi sasa si nzuri sana na tumeona busara kuachana na Pluijm ili mambo mengine yaende.”
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV