April 20, 2017Beki wa Simba, Abdi Banda amesema hakufurahia yeye kumpiga ngumi kiungo mkongwe wa Kagera Sugar, George Kavila.

Banda amefungiwa kucheza mechi mbili baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga ngumi Kavila na tayari ameishaitumikia adhabu hiyo.

"Haya ni mambo ya mpira, anayecheza mpira anaweza akanielwa. Mnaweza kutofautiana lakini baada ya hapo, mnaelewana.

"Nilishamuomba msamaha na yeye alielewa, ninaamini tunaweza kuendelea," alisema.

Katika mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo Simba ililala kwa mabao 2-1, Banda alimtwanga ngumi Kavila wakati wakiwa hawana mpira.

Taarifa za ndani kutokana kamati iliyompa adhabu zimeelezwa, kitendo cha Banda kumuomba radhi Kavila, kilichangia yeye kupunguziwa adhabu.

Kwa kuwa alikosa mechi dhidi ya Mbao FC na Toto African, sasa yuko huru kuendelea kuitumikia Simba.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV