April 20, 2017Stand United imeshinda mechi yake ya Ligi Kuu Bara baada ya kuitwanga Ndanda FC kwa mabao 3-0.

Mechi hiyo imechezwa kwenye Uwanja wa Kambarage katika Manispaa ya Shinyanga.

Stand United ilitawala mchezo huo kuanzia kipindi cha kwanza na Jacob Massawe ndiye alianza kuandika bao kabla ya Frank Hamis kuongeza la pili na baadaye la tatu.


Stand United imeonyesha ina nia ya kubaki Ligi Kuu Bara na Kocha Bilal Billo amesema wamejiondoa katika hofu ya kuporomoka daraja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV