April 20, 2017
Mtanzania Mbwana Samatta atakuwa na jukumu gumu kuhakikisha timu yake ya KRC Genk inavuka mtihani wa Celta Vigo inayoshiriki La Liga.

Mechi hiyo inayomhusisha Samatta ambaye watangazani kadhaa wa runinga mbalimbali wamekuwa wakilitamka jina lake "Bwana Samatta", itaanza saa 4:05 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Celta Vigo ilishinda kwa mabao 3-2 katika mechi yake ya kwanza ya Europa League ikiwa nyumbani.

Genk ikiwa nyumbani na Samatta akiwa na jukumu la kuongoza mashambulizi, itakuwa inataka kuvuka.

Kocha wake ameamua kutumia mfumo wa 4-2-3-1 ambao unamfanya Samatta kubaki mbele peke yake huku Siebe Schrivers, Alejandro Pozuelo na Leandro Trossard wakiwa wanamsaidia.

Haitakuwa kazi rahisi hasa Celta Vigo yenye washambulizi matata kama Iago Aspas, John Guidetti na Pione Sisto.

Lakini Samatta hana ujanja, ni lazima apambane kweli na kutoa msaada mkubwa.


Kama mambo yataenda vizuri na Genk ikaing’oa Celta Vigo, hakika thamani ya wachezaji kadhaa wa Genk akiwemo Samatta lazima itapaa na watakuwa na nafasi ya kukutana na timu nyingine kubwa na maarufu hali itakayowasaidia kupata soko zaidi. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV