April 24, 2017


Kiungo wa Chelsea, N’Golo Kante ameibuka mshindi katika tuzo ya mchezaji bora wa kulipwa nchini England.

Kante amechukua ushindi mbele ya wachezaji wengi nyota ambao walikuwa wakipewa nafasi kama Eden Hazard (Chelsea), kutoka Tottenham’, Harry Kane, Zlatan Ibrahimovic (Manchester UnitedI, Romelu Lukaku (Everton)na Alexis Sanchez wa Arsenal.

Kante 26, ambaye ni raia wa Ufaransa ameshinda tuzo hiyo ambayo hutolewa na chama cha wanasoka wa kulipwa.

Chelsea ilimwaga kitita cha pauni milioni 32 kumnasa Kante kutoka Leicester aliyokuwa ameisaidia kuipa ubingwa msimu uliopita.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic