April 25, 2017



Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina anaamini kikosi chake kina nafasi ya kuendelea kufanya vizuri.

Lwandamina raia wa Zambia, alifurahishwa na kiwango walichokionyesha Yanga katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Prisons ya Mbeya.

Lakini amesisitiza, wataendelea kufanya vizuri na kikubwa ni kuendelea kujituma.

“Mpira ni ushindani na kila siku lakini ujitume mazoezini, ujitume katika mechi. Ninaamini bado tuna nafasi ya kuendelea vizuri,” alisema.


Yanga ilionyesha kiwango kizuri na kuitwanga Prisons kwa mabao 3-0 katika mechi iliyokuwa ikitarajiwa kuwa ngumu kwa Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic