April 25, 2017



Nyota wa zamani wa Yanga na Simba, Edibily Lunyamila amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufanya mambo kwa weledi badala ya kuangalia maslahi binafsi kwa viongozi wake.

Lunyamila ambaye alikuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha timu ya taifa, amewataka TFF kuachana na ushabiki katika masuala ambayo yanahusiana na haki.

“Sitaki kuingia au kukaa upande wowote katika suala la Simba na Kagera kuhusiana na pointi tatu. Lakini ninachosisitiza ni TFF kufanya mambo kwa uwazi.

“Hili suala lilikuwa lina figisu nyingi tokea mwanzo, lakini TFF hawakuonekana ni watu waliotaka liishe kwa uwazi kwa kuanika mambo hadi serikali ilipoingilia.

“Hii si sawa, inasababisha watu wengi zaidi kuendelea kupoteza kabisa imani na TFF,” alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic