April 14, 2017

MKEMI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI, LEO.


Uongozi wa Yanga umesema hautaenda mahakamani kupinga Simba kupewa pointi tatu.

Simba imeshinda rufaa yake dhidi ya Kagera Sugar na kupata pointi tatu na mabao matatu ikiwa ni baada ya kubainika beki Mohamed Fakhi alicheza mechi dhidi ya Simba akiwa na kadi tatu za njano.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amesema kama kuna wanachama wanataka kwenda mahakamani, wao hawatakuwa na uwezo wa kuwazuia huku akisisitiza Tanzania ikifungiwa, Serengeti Boys itang’olewa kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika na ile kauli mbio ya Gabon mpaka Kombe la Dunia itageuka na kuwa “Gabon hadi Nyumbani Tanzania”.


“Wakiendelea hivi itakuwa ni Gabon hadi Nyumbani, haitakuwa Kombe la Dunia tena.

”Watu wana hasira zao, sisi viongozi tunaweza tusijue kinachoendelea. Kagera ni timu ndogo, wanaonewa, hawatendewi haki. Sasa sisi tumeinunua hii kesi.


“Ajabu kabisa, waamuzi wameitwa wawili tu na wengine hawakuitwa. Hii si sawa, kuna jambo hapa,” alihoji Mkemi akionekana ni mwenye jazba.

2 COMMENTS:

  1. Mara nyingine waadishi wetu mnapaswa mtoe Elimu ya "uraia wa kanuni za soka", yawezekana mwenzetu huyu hajuwi taratibu za kuiondoa nchi katika mashindano.Kabla ya Tanzania kufutiwa uwanachama,TFF itaifutia yanga uanachama,sasa chama cha soka kinapomuwajibisha mwanachama wake mtovu wa nidhamu,CAF na FIFA wataiadhibu vipi Tanzania katika mambo ambayo shirikisho letu limeshachukua hatua?

    Yanga ikilipeleka suala hili mahakamani inafutwa yenyewe,si Serengeti Boys.Mkemi aache kuwapotosha wenzake.Mbona simba ilipopokwa point 3 ikapewa Kagera kwa kosa la kumchezesha Mgosi akiwa Na kadi 3 za njano yanga haikupiga kelele?Azamu ilipopokwa point na kupewa Mbeya City Mbona hatukumsikia mkemi akipaza sauti?

    Kagera wamefanya kosa la kikanuni na wameadhibiwa kwa mujibu wa kanuni,sasa kelele za nini?Yanga icheze mpira,iache visingizio,kelele hazitawasaidia kitu,wakienda mahakamani iwe viongozi au wanachama,klabu ya yanga itatelemshwa daraja na kwenda kucheza ndondo cup na kina kauzu FC.Kinacholiondoa Taifa ni migogoro ya chama cha soka na serikali,si chama cha soka na mwanachama wake(klabu),Mwanachama anayekiuka taratibu na kanuni atawajibishwa kwa mujibu wa taratibu na kanuni,na si vinginevyo.Yanga ikikimbilia mahakamani itafutwa yanga na si Serengeti boys.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV