April 14, 2017


Yanga imetangaza kutokuwa na imani tena na watendaji na wafanyakazi wote ndani ya bodi ya Ligi.


Hilo limetangazwa na uongozi wa Yanga kupitia mjumbe wa kamati ya klabu hiyo, Salum Mkemi.


Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo, Mkemi amesema wafanyakazi wa bodi hiyo wanapaswa kufukuzwa.


“Waamuzi wameondolewa kutokana na tuhuma, tumeshangazwa na mashaka na hatuna imani na watendaji wa bodi ya ligi, hadi mtendaji mkuu.



“Vipi wanashindwa kuwa na kumbukumbu, eti walienda kumuita mwamuzi atoe ufafanuzi. Je, angekuwa mgonjwa au alishafariki? Kuwapa Simba pointi tatu, inaonyesha wanapaswa kuwajibishwa na kufukuzwa mara moja,” alisema Mkemi akionekana ana jazba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic