Mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema mabao 100 aliyofunga Ulaya ni jambo ambalo hakulitegemea.
Ronaldo raia wa Ureno, ameweke rekodi kwa kufikisha mabao 100 aliyofunga barani Ulaya.
“Si jambo dogo, si jambo rahisi. Sikuwahi kutarajia hili kwamba siku moja nitafikisha mabao 100,” alisema.
Ronaldo alisema ameshangazwa pia kusikia kwamba kuna ambao walikuwa na hofu kuhusiana na uwezo wake wa kufunga mabao kwa kuwa umri wake sasa ni zaidi ya miaka 30.
0 COMMENTS:
Post a Comment