April 14, 2017



Pamoja na juhudi za vigogo wa Klabu ya Yanga kumshawishi mshambuliaji wao, Obrey Chirwa raia wa Zambia kuungana na wenzake kuelekea nchini Algeria kuwavaa MC Alger ya nchini humo, taarifa kutoka ndani ya viongozi hao ni kuwa mshambuliaji huyo hakupatikana hewani baada ya kufunga simu zake zote.

Chirwa aliyejiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea FC Platinum ya Zimbambwe, aligoma kuungana na wenzake kwa ajili ya safari hiyo kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya MC Alger kwa kile kinachodaiwa kutokulipwa kwa mishahara yake ya miezi mitatu.

Habari za uhakika ni kuwa baada ya Chirwa kugoma ndipo jina lake likaondolewa katika orodha ya waliotakiwa kusafiri kwenda Algeria, jana jioni.

“Jana (juzi) kuna vigogo wa Yanga ambao sitapenda kuwataja majina yao walikuwa wakimtafuta Chirwa ili kumshawishi aungane na wenzake katika safari lakini simu zake zote za mkononi zilikuwa hazipatikani,” kilisema chanzo na kuendelea:

“Kuna waziri alinipigia simu akiniulizia ishu hiyo nikamueleza mimi ninavyojua, hivyo akaniomba nimtafute Chirwa ili aweze kuzungumza naye ikiwezekana aungane na wenzake ila imeshindikana maana nilimpigia Chirwa sikumpata, nilipoenda nyumbani anapoishi sikumkuta.”


Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, alisema: “Chirwa hajaungana na wenzake kwa kuwa ana matatizo yake ya kifamilia.” 

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic