April 28, 2017

MHARIRI MTENDAJI WA GLOBAL PUBLISHERS LTD, SALEH ALLY (WA PILI KULIA), AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI HAO PAMOJA NA BAADHI YA VIONGOZI WAO.

Wanafunzi wenye vipaji mbalimbali kutoka nchini Kenya, leo wametembelea ofisi za uchapishaji magazeti za Global Publishers Ltd eneo la Bamaga jijini Dar es Salaam.

Wanafunzi hao waliongozwa na Ofisa Mawasiliano wa kampuni ya Africa Nasaha Production ya nchini Kenya, Oscar Njeru walijifunza mambo kadhaa ya uandaaji wa magazeti ya Championi, Ijumaa na mengineyo.

Lakini pia walijifunza namna kazi ya utafutaji habari, zinavyopandishwa mitandaoni na pia kazi zinazofanywa na Global TV online, runinga ya mtandaoni inayofanya vizuri zaidi kipindi hiki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV