May 15, 2017
Uongozi wa Simba umepanga kukutana na Mohamed Dewji na kumaliza tofauti zao.

Dewji maarufu kama Mo, aliamua kujitoa katika suala la mchakato wa mabadiliko baada ya klabu ya Simba kuingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya ubashiri ya SportPesa.

Mo alionyesha kukasirishwa baada ya uongozi kutomshirikisha yeye pamoja na wajumbe wengine wa kamati ya utendaji, jambo aliloliita kutoaminiana miongoni mwao.

“Uongozi utakutana na Mo, itakuwa leo au kesho ili kulimaliza suala hilo. Kinacholengwa ni kuonyesha busara baada ya matatizo yaliyotokea.

“Kama ambavyo umeona, uongozi umefika kwa Hans Poppe, umekaa na kuzungumza naye na suala limefikiwa kwa kupatikana muafaka.


“Sasa ni lazima kukutana na Mo, Simba hatutaki mifarakano,” kilieleza chanzo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV