May 14, 2017Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amemuorosha mshambulizi Donaldo Ngoma katika idadi ya washambulizi anaowataka msimu ujao.

Hali hiyo imeonekana kuwashangaza baadhi kwa kuwa wanaamini Ngoma ataondoka na tayari mapenzi ya Wanayanga yameanza kuondoka kwake.

Mkataba wa Ngoma umebakiza mwezi mmoja tu kuisha na uongozi wa Yanga ulitangaza kwamba mchezaji anayetaka kuondoka ruksa na kumekuwa na taarifa kuwa Ngoma yuko kwenye rada za watani wao Simba.

Taraifa za ndani kutoka Yanga, zimeeleza, Lwandamina anataka mshambulizi mwenye usumbufu kama wa Ngoma kwa kuwa anakuwa anwachosha mabeki kama ilivyo kwa Jesse Were raia wa Kenya ambaye anakipiga Zesco ya Zambia aliyokuwa anaifundisha kabla ya kutua Yanga.

"Unaona Chirwa anaanza kuimarika, ni msumbufu lakini anatokea pembeni. Kocha angependa kupata mchezaji msumbufu pia katikati ya uwanja.

"Anaamini hiyo itampa nafasi ya mchezaji kama Tambwe kufunga kwa urahisi. Naamini wamezungumza na Ngoma," kilieleza chanzo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV