May 28, 2017


Baada ya kuingoza Barcelona kubeba ubingwa wa Copa del Rey, Andres Iniesta ameweka rekodi mpya ya kuwa mchezaji aliyebeba makombe mengi kuliko mwingine yoyote wa Hispania.

Iniesta amefikisha makombe 33 tofauti na kumpita kwa kombe moja, Xavi Hernandes ambaye walikuwa kabla wanalingana kwa makombe 32 kila mmoja.

Barcelona iliitwanga Alaves kwa mabao 3-1 na kufanikiwa kubeba ubingwa huo wa Copa del Rey maarufu kama Kombe la Mfalme.

Kombe hilo limekuwa ni la tano la Iniesta kwa Copa del Rey, ni kombe lake la 30 kwa makombe ya ndani.


Amebeba makombe nane ya La Liga, makombe manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, pia ana Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, pia Kombe la Mataifa Ulaya maarufu kama Euro, mara mbili 2008 na 2012.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV