May 28, 2017



Nahodha wa Simba, Jonas Mkude amefikishwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam na kufanyiwa vipimo.

Mkude alikuwa kati ya watu sita waliopata ajali iliyotokea leo na shabiki mmoja wa Simba, Shose Fidelis amepoteza maisha.

Lakini Mkude na abiria wengine walipata majeraha huku Mkude alilalama kuhusiana na kuumia shingo na kichwa.

Hata hivyo, mmoja wa wajumbe wa kamati ya Utendaji ya Simba, Muslah Al Rawah, amesema Mkude amepatiwa matibabu.

"Amefanyiwa vipimo Muhimbili, yupo hapo na matibabu yanaendelea," alisema.

"Uongozi uko naye karibu pamoja na majeraha wengine pamoja na familia ya shabiki aliyepoteza maisha," alisema.

Gari walilokuwa wamepanda akina Mkude lilikuwa likiendeshwa na shabiki wa Simba aitwaye Presdaa na lilipata ajali baada ya tairi kupasuka katika eneo la Dumila.

Mkude na wenzake walikuwa safari kurejea Dar es Salaam baada ya Simba kuishinda Mbao FC kwa mabao 2-1 na kubeba Kombe la Shirikisho la Azam Sports.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic