May 21, 2017


Taarifa za nahodha wa Azam FC na mshambulizi tegemeo, John Bocco kuwa ametemwa Azam FC zimeenea kila sehemu mitandaoni.

Kumekuwa na taarifa kwamba Azam FC wameamua kuachana na Bocco ambaye ameichezea timu hiyo tokea ianzihwe.

Ambacho kinaonekana kuwashitua mashabiki ni Bocco kutupia maneno kadhaa mtandaoni ya kijamii katika akaunti zake yanayoashiria kuaga au kuondoka.


Hata hivyo, SALEHJEMBE imefanya juhudi na kupata uhakika kutoka ndani ya Azam FC na kugundua kuwa mkataba wa Bocco umemalizika.

“Ni kweli mkataba wa Bocco umeisha na sasa yuko katika mazungumzo na uongozi.

“Suala la kwamba anaondoka sijalisikia, lakini najua wanazungumza,” kilieleza chanzo.

Juhudi za kumpata Bocco, kumekuwa na ugumu lakini alipatikana Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi ambaye naye alitoa ufafanuzi wake.

“Suala la mchezaji kuingia katika mazungumzo na klabu ni la kawaida.

“Kuhusu mkataba wake na klabu inabaki kuwa siri ya hizo pande mbili lakini hakuna taarifa za Bocco kuachwa,” alisema.









0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic