May 21, 2017


Inaonekana Kocha Jose Mourinho ameanza kufanya juhudi kuhakikisha anampata mshambulizi Zlatan Ibrahimovic katika fainali ya Kombe la Europa dhidi ya Ajax.

Fainali ya Europa itachezwa Mei 24 jijini Stockholm, Sweden ambako ni kwao Zlatan na Ajax ni timu yake ya kwanza kubwa kucheza nje ya Sweden.

Zlatan ambaye aliumia vibaya goti lake, tayari ameanza mazoezi maalum yakiwemo yale ya ndani ya maji ili kuhakikishaa napona haraka.


Hivi karibuni, Zlatan alifanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Pittsburgh na amekuwa akiendelea vizuri.

Juhudi hizo za sasa ni kujaribu kumpata ili kuwa na mtu wa uhakika.

Hivyo Zlatan amekatisha mapumziko yake ili kujaribu kurejea kwa kupitia matibabu hayo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic