May 6, 2017


MPIRA UMEKWISHAAAA
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA

KULE MWANZA TOTO 2-1 JKT RUVU, MPIRA UMEISHA NA JKT UNAWEZA KUSEMA NI ASILIMIA 85 WANATEREMKA DARAJA
KULE UWANJA WA MABATINI MLANDIZI RUVU SHOOTING 1-1 KAGERA SUGAR (FULL TIME)

Dk 88, Mwashiuya anachonga kona ya 13 ya Yanga katika mchezo huu, lakini mpira unaokolewa hapa

Dk 87 Yanga wanapata kona tena baada ya walinzi Prisons kulazimika kutoa, inachongwa na Niyonzima, Kalambo anaokoa na kuwa kona nyingine
SUB Dk 85 Prisons wanamuingiza Kazungu kuchukua nafasi ya Samatta


Dk 85, Yanga wanavyokwenda wanaweza kupata bao la tatu, Prisons wanavyocheza wanaonekana wanazuia zibaki hizi mbili maana hawana uwezo tena wa kufunga
Dk 82 Matheo anatoa pasi nzuri kwa Msuva lakini kipa Kalambo anawahi na kuudaka
SUB Dk 81 Chirwa anakwenda kwenye benchi na nafasi yake inachukuliwa na Matheo Anthony
SUB Dk 80, anaingia Freddy Chudu kuchukua nafasi ya Meshack Selemani


GOOOOOOO Dk 75 Chirwa anapiga kichwa kuujaza mpira wavuni akiunganisha mpira wa kichwa wa Tambwe
Dk 73, Chirwa anajaribu vizuri kabisa hapa lakini Kalambo yuko makini, anaokoa
Dk 72 Yanga wanapata kona nyingine baada ya Msuva kuingia vizuri lakini mpira ukaokolewa
GOOOOOOOOOOO  Dk 70, krosi safi ya Juma Abdul, Tambwe anaandika bao safi kwa kichwa
Dk 69 Hangaya anafanya kazi ya ziada anaokoa na mpira unamgonga Tambwe na kuwa goalkick
Dk 68 shuti la Chirwa linaokolewa na kuwa kona upande wa Prisons

SUB Dk 66 Yanga wanafanya mabadiliko, anaingia Haruna Niyonzima kuchukua nafasi ya Said Juma Makapu
Dk 65 Mwashiuya anaachia mkwaju mkali kabisa lakini mpira umegonga nyavu za nje
Dk 64  Kassim Hamis anaingia na kuachia shuti kali baada ya kutengewa na Meschack lakini Goal Kick
Dk 63, hawa Prisons wote wamerudi nyuma na inavyoonekana hii itachangia wao kufungwa. Wanavyocheza utafikiri ni dakika ya 85 wakati muda bado ni mwingi sana na hatari kwao

SUB Dk 63 Kassim Hamis anaingia kuchukua nafasi ya Hangaya upande wa Prisons
KADI Dk 62, Yondani anamuangusha Hangaya na analambwa kadi ya njano
SUB Dk 59 Yanga wanafanya mabadiliko ya kwanza kwa kumtoa Kessy na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Abdul
Dk 57, Nusura Kessy ajichanganye lakini Kakolanya anatokea na kuokoa kwa kasi hapa
Dk 55 Selemani yeye na lango anasgindwa kumalizia hapa, ilikuwa ndiyo nafasi bora zaidi ya Prisons


KADI Dk 53 Kessy analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Meshack Selemani ambaye amekuwa akimpa wakati mgumu
Dk 51, mpira safi wa faulo wa Msuva, Makapu anaukosa kidogo tu kuusukumiza wavuni
Dk 47, Kamusoko anasogea karibu na 18 na kuachia shuti lakini kipa Prisons anauona na kudaka vizuri kabisa
Dk 46, Mwashiuya anaachia mkwaju mkali wa adhabu lakini kipa kalambo anaokoa na kuwa kona. Inachongwa hapa lakini haina madhara
Dk 46, Yanga wanapata mkwaju wa adhabu nje ya eneo la 18 la Prisons

KULE MWANZA TOTO 2-1 JKT RUVU, SASA NI DAKIKA YA 50 SASA

Dk 45, mechi imeanza na inaonekana Yanga wanataka kupata bao la mapema


MAPUMZIKO
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 44, Asukile analazimika kuokoa krosi safi ya Mwinyi Haji
Dk 43 Yondani yuko chini pale anatibiwa, ni baada ya kugongwa na Lambert
Dk 40 Yanga wanapata kona tena lakini kipa Kalambo yuko makini kabisa
DK 38, Msuva anaruka na kupiga kichwa cha chinichini
Dk 37 Yanga wanapoteza nafasi nzuri kabisa baada ya Msuva kuukosa mpira akiwa yeye na kipa
Dk 35 inachongwa kona hapa, Kamusoko anaachia shuti lakini ni faulo, kipa Kalambo yuko chini
Dk 34 kipa Kalambo Aaron anafanya kazi ya zaida kuokoa shuti kali la mpira wa adhabu wa Mwashiuya,kona
Dk 33, Yanga wanapata faulo nje kidogo ya 18 baada ya MWashiuya kuangushwa
Dk 32 Yanga wanafanya shambulizi kali hapa, shuti la Bossou linaokolewa na kuwa kona

KULE MWANZA TOTO 1-1 JKT RUVU, SASA NI DAKIKA YA 34

KADI Dk 31 Nurdin Chona wa Prisons analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Mwahiuya
Dk 30, Kamusoko anaachia mkwaju mkali hapa lakini Samatta anachukua mpira na kuondoka nao
Dk 29, Kimenya anamuacha Mwinyi Haji hapa lakini krosi yake inakuwa hovyo kabisa
KADI Dk 26, Benjamini Asukile analambwa kadi ya njano kwa kumuangisha Msuva katikati ya uwanja
Dk 25 Msuva anaangushwa hapa, mwamuzi anasema hii ni kazi ya wanaume, twende tusonge
Dk 23, krosi nyingine Kessy lakini kipa Aaron wa Prisons anadaka vizuri kabisa

Dk 19, krosi nzuri ya Ismail lakini Hangaya anajichanganya na mpira unakuwa goal kick
Dk 14 sasa, zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja kila timu ikiwa makini katika ulinzi
Dk 8, Yanga wanapata kona ya tatu baada ya Ismail kulala na kuondosha hatari, inachongwa na Kamusoko hapa, almanusura lakini Prisons wanaokoa hapa
Dk 7, Prisons wanatoa tena na inakuwa kona ya pili ya Yanga, Mwashiuya anaichonga lakini Msuva anajigonga na Prisons wanaokoa

Dk 4, Chirwa akiwa mbali anaachia mkwaju hapa, goal kick
Dk 3, Selemani wa Prisons anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, goal kick
Dk 2, Benjamin Asukile analala na kuokoa, inakuwa konaaa ya kwana kwenda lango la Prisons, inachongwa na Mwashiuya na Mwasukile anaondosha tena
Dk 1, Prisons wanaanza kwa kasi lakini Yanga wanakuwa makini, wanaokoa na kwenda kwa kasi langoni mwao lakini Prisons wanaokoa pia

MWAMUZI: Selemani Kinugani-Morogoro
REKODI
Leo Yanga na Prisons zinakutana mara ya 12
Yanga imeshinda 7
Sare 4
Prisons imepoteza 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV