May 6, 2017


Pamoja na kuwa kuwa majeruhi, mshambuliaji mkongwe wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic, 35, amepaa na kushika nafasi ya pili kwa wanamichezo wanaoingiza kipato kikubwa zaidi kwa mwaka nchini Uingereza.

Listi hiyo inajumuisha wanamichezo wote wa Uingereza wlaio ndani na nje ya nchi hiyo zikijumuishwa Wales na Ireland pia Scotland. Hii ni kwa michezo yote na haijali uraia wa mwanamichezo mwenyewe.

Lewis Hamilton dereva wa nagari ya langalanga au formula 1 anaendelea kushika namba moja akiwa amekusanya kitita cha pauni million 131 kwa mwaka.

Zlatan raia wa Sweden yeye amepaa hadi kufikisha pauni million 110 kwa mwaka na kumshusha nahodha wake Wayne Rooney. Hii inatokana na kipato cha Zlatan kuongeza zake kwa haraka kwa pauni milioni 25.
Rooney aliyekuwa anashika namba mbili, ameendelea kubaki na pauni million 93 kwa mwaka. Hivi karibuni, Zlatan alikataa kulipwa mshahara wake kwa madai kwamba hawezi kuchukua mshahara wakati hatakuwa akicheza hadi msimu ujao.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV