May 17, 2017



WACHEZAJI WATANO KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA 



Wachezaji watano wameteuliwa (nominees) kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2016/2017.

Walioteuliwa kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho ni Aishi Manula (Azam FC), Haruna Niyonzima (Yanga), Mohamed Hussein Zimbwe (Simba), Shiza Kichuya (Simba) na Simon Msuva (Yanga).

Amissi Tambwe amekuwa hana msimu mzuri na anaonekana kukosa nafasi hiyo lakini wengi wamehoji kuhusiana na Mbaraka Yusuf wa Kagera Sugar.

Majina hayo yatapigiwa kura na makocha, makocha wasaidizi na manahodha wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na wahariri wa michezo kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Wahusika watatumiwa fomu maalum za kupiga kura kwenye email za klabu zao na vyombo husika vya habari. Mwisho wa kupiga kura ni saa 6 usiku ya Jumanne, Mei 23 mwaka huu.


Hafla ya kutoa tuzo hiyo ambayo inaratibiwa na Kamati ya Ushauri ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanyika Mei 24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV